Saturday 5 March 2022

JUHUDI ZA KUPIGA VITA UVUVI HARAMU KWA NJIA SHIRIKISHI YA JAMII YAANZA KUZAA MATUNDA:

Wanakijiji wa kijiji cha Stahabu Wilayani Pangani Mkoani Tanga watoa mfano wa kuigwa kwenye CFMA ya USTASAKI  kwa kujikita zaidi kwenye uvuvi wa madema na kuachana na aina nyinginezo za uvuvi haramu uliokuwa tishio kwa maeneo hayo licha ya ugumu wa maisha unaowakabili.

Juhudi mbalimbali za uelimishwaji juu ya uvuvi endelevu zinazotolewa na taasisi mbalimbali kwa njia shirikishi ya jamii  Wilayani humo zaanza kuzaa matunda hii ni baada ya kuwashuhudia mabadiliko na jitihata zilizoonekana miongoni mwa wanajamii hawa,wake kwa waume wakijishughulisha zaidi na shughuli za utengenezaji madema ikiwa kama moja kati ya mitego yao tegemezi ya shughuli zao za uvivi za kila siku.

Hii imeonekana siku ya Alhamisi mwakilishi wa AAS alipowatembelea bila taarifa na kuwakuta wakifanya shughuli hizi na kufanya mahojiano nao kwa muda mfupi.


Wito na ushauri toka kwa Jamii hizi:

  • Waungwe mkono ktika kuhakikisha jitihada hizi zina zaa matunda na pia zinakuwa endelevu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kichacho.
  • Elimu ya zana na uvuvi endelevu iendelee kutolewa zaidi ili kutokomeza kabisa uvuvi haramu.
  • Vikundi mbali mbali vya wavuvi wawezeshwe kupata zana bora za uvuvi zenye kuzingatia suala zima la uvuvi endelevu.
  • Ushirikishwaji wa jamii uzidishwe hususani kwenye mbambo mbalimbali ikiwemo mikakati ya kulinda na kutunza rasilimali zao ili kutia mchango wao.  


 Omary ni moja kati ya vijana wakazi wa kijiji hichi,pia ni moja kati ya vijana wenye moyo wa kujituma kuhakikisha uhifadhi unatekelezwa hususani katika jamii yake,pia hakuwa alikuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa zoezi hili.

No comments:

Post a Comment