Wednesday 2 January 2019

UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA VIZIMBA

 UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA VIZIMBA

(FLOATING NET CAGE FISH FARMING)


    Hii ni aina ya ufugaji samaki kwa kutumia vizimba/cages.Vizimba hivi huwa vya maumbo tofauti tofauti kama mraba,mstatili na umbo la pipa.  

Ndani ya vizimba hivi ndimo samaki hufugwa,vizimba hutegwa majini eidha kwenye maziwa,mabwawa,baharini ama mtoni. Baada ya hapo samaki hufugwa humo mpaka wakati wa uvunaji.

Aina hii ya ufugaji pia kwa lugha ya kigeni inapofanyika kwenye vyanzo vya maji vya asili hujulikana kama off-shore cultivation/outdoor fish farming  ikifanyika  baharini.

             MUONEKANO WA UFUGAJI WA KUTUMIA VIZIMBA ZIWANI                               (FLOATING NET CAGE FISH FARMING) 

                           

Moja ya wataalamu wa ufugaji samaki kutoka AAS ndugu Donald Kusekwa Masondole akitembelea mradi na kushiriki zoezi la ulishaji samaki  na kutoa ushauri wa kitaalamu:
 
 
>>Faida za aina hii ya ufugaji hasa ukifanyika baharini,mitoni na maziwani:

   *Samaki hawawezi kupata mabadiliko ya joto mwilini kirahisi kwani eneo lenye maji(space) inakuwa ni kubwa hivyo hufanya uwepo wa hewa ya oxygen ya kutosha ndani ya kizimba,uwepo wa hali joto isiyo panda ghafla na kushuka kupita kiasi( extremely temperature fluctuation).

    *Uwepo wa chakula cha asili cha kutosha (Algae,Phyto  plankton,Zoo Plankton).

   *Pia uwepo wa maji mengi yaliyo kwenye mwendo kutokana na mawimbi ama mkondo husaidia sana  kwenye suala la uzalianaji kwa aina ya samaki wasio zaliana kwenye maji yaliyo simama(stagnant water).

Hivi vyote kwa pamoja hupelekea ukuaji wa samaki aneyefugwa kwa aina hii ya ufugaji kukua vizuri na kwa haraka kuliko yule anayefugwa kwenye bwawa.


>>Udhaifu wa njia hii ya ufugaji kwa mimea na viumbe  waishio baharini,mitoni na maziwani (Negative effect of Cage fish farming in the aquatic biodiversity):


    *Aina hii ya ufugaji yaweza kuwa hatari kimazingira endapo mfugaji hatakuwa makini yaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira ya majini,fukwe na viumbe waishio majini kwa ujumla,endapo  mfugaji hata kuwa makini katika suala la kuzingatia ubora/viwango vya vifaa alivyotumia kutengenezea cages zake ama kuzingatia muda sahihi wa kubadili vifaa hivyo na kuweka vipya.vitu kama nyavu za plastic na plastic materials nyingine anazotumia kwenye ufugaji vikiharibika ama kwa bahati mbaya kuingia majini huweza kuathiri maisha ya viumbe waishio kwenye vyanzo hivyo vya maji.

    * Pia Utumiaji wa kemikali katiki uzalishaji,ukuzaji na kutibu ama kinga si mzuri kufanya katika aina hii ya ufugaji,kemikali hizo huweza kuathiri viumbe na mimea wanaopatikana katika chanzo hicho cha maji na hata kukaribisha uwepo wa viumbe wapya na hatarishi kwa viumbe wa zamani.
 
>>Udhaifu wa kiuchumi(economic effect):


    *Pia aina hii ya ufugaji ni chaguzi (selective),ni rahisi zaidi kwa watu waishio pembezoni mwa vyanzo vikubwa  vya asili vya maji.

    *Lakini pia aina hii ya ufugaji unagharama kidogo Zaidi ya ule wa mabwawa kwa upande wa miundombinu yake.

 

1 comment: