FAHAMU AINA KUU ZA MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI
Kuna aina kuu mbili za mabwawa:
1. Bwawa la Udongo
2. Bwawa la Simenti
1.(a)Bwawa la udungo husakafiwa na udongo wa mfinyanzi unaohifadhi maji kwa mda mrefu bila kuruhusu upotevu wa maji ardhini.
b)Bwawa la udongo lililotandikwa karatasi maalumu ya plastic:
Kwa eneo lisilokuwa na udongo mzuri unaoweza kuhifadhi maji kwa muda mrefu ni vizuri ukatengeneza aina hii ya bwawa ili kuepusha hasara ya upotevu wa maji mara kwa mara.
Hizi ni Baadhi ya faida na hasara za bwawa la udongo:
Faida:
➧Hupunguza gharama za ulishaji kwa mfugaji kwakua samaki hujipatia chakula cha asili ndani ya bwawa.
➧Gharama zake za ujenzi ni ndogo ukilinganisha na bwawa la simenti.
➧Halihitaji ujuzi mkubwa sana wa ujenzi ukilinganisha na bwawa la simenti.
➧Gharama za kukuza samaki kwa bwawa la udongo ni ndogo kwakua ndani ya bwawa la udongo kunauzalishwaji mkubwa wa hewa safi pia kiwango cha joto si kikubwa hasa kwa bwawa la udongo wa ufinyanzi lisilokuwa na plastic hivyo huwafanya samaki wakue vizuri na kwa haraka na bia humpunguzia mfugaji gharama za ziada za kununua vizalishaji hewa(aerator).
Hasara:
➧Sio imara sana ukilinganisha na bwawa la siment.
➧Usipokua makini wakati wa uchaguzi sahihi wa eneo la ujenzi wa bwawa lenye udongo unaohifadhi maji vizuri unaweza pata hasara ya upotevu wa maji mara kwa mara.
2. Bwawa la simenti hili husakafiwa kwa simenti na hutengenezwa kwa tofali,simenti,kokoto,nondo na matirio mengine.Ujenzi wa bwawa hili kidogo ni wagharama ukilinganisha na bwawa la udongo kwakuwa linahitaji vifaa vingi zaidi.
FAHAMU AINA KUU ZA MABWAWA YA KUFUGIA SAMAKI
Kuna aina kuu mbili za mabwawa:
1. Bwawa la Udongo
2. Bwawa la Simenti
1.(a)Bwawa la udungo husakafiwa na udongo wa mfinyanzi unaohifadhi maji kwa mda mrefu bila kuruhusu upotevu wa maji ardhini.
(b)Bwawa la udongo lililotandikwa karatasi maalumu ya plastic:
Kwa eneo lisilokuwa na udongo mzuri unaoweza kuhifadhi maji kwa muda mrefu ni vizuri ukatengeneza aina hii ya bwawa ili kuepusha hasara ya upotevu wa maji mara kwa mara.
Hizi ni Baadhi ya faida na hasara za bwawa la udongo:
Faida:
➧Hupunguza gharama za ulishaji kwa mfugaji kwakua samaki hujipatia chakula cha asili ndani ya bwawa.
➧Gharama zake za ujenzi ni ndogo ukilinganisha na bwawa la simenti.
➧Halihitaji ujuzi mkubwa sana wa ujenzi ukilinganisha na bwawa la simenti.
➧Gharama za kukuza samaki kwa bwawa la udongo ni ndogo kwakua ndani ya bwawa la udongo kunauzalishwaji mkubwa wa hewa safi pia kiwango cha joto si kikubwa hasa kwa bwawa la udongo wa ufinyanzi lisilokuwa na plastic hivyo huwafanya samaki wakue vizuri na kwa haraka na bia humpunguzia mfugaji gharama za ziada za kununua vizalishaji hewa(aerator).
Hasara:
➧Sio imara sana ukilinganisha na bwawa la siment.
➧Usipokua makini wakati wa uchaguzi sahihi wa eneo la ujenzi wa bwawa lenye udongo unaohifadhi maji vizuri unaweza pata hasara ya upotevu wa maji mara kwa mara.
2. Bwawa la simenti hili husakafiwa kwa simenti na hutengenezwa kwa tofali,simenti,kokoto,nondo na matirio mengine.Ujenzi wa bwawa hili kidogo ni wagharama ukilinganisha na bwawa la udongo kwakuwa linahitaji vifaa vingi zaidi.
Baadhi ya faida na hasara za ujenzi wa bwawa la siment:
Faida:
➧Ni imara,hudumu kwa muda mrefu ukilinganisha na bwawa la udongo.
Hasara:
➧Utengenezwaji wake ni wa gharama zaidi ukilinganishasa na bwawa la udongo,linatumia vifaa vingi na vya gharama.
➧Pia linahitaji utaalamu zaidi wa usimamizi wakati wa ujenzi.
➧Ndani ya bwawa la simenti uzalishwaji wa chakula cha asili,hewa safi huwa mdogo ukilinganisha na bwawa la udongo hivyo humuongezea mkulima gharama za ulishaji.
➧Hatari ya mabadiliko ya kiwango cha joto ndani ya bwawa la simenti na lile lililo tandikiwa karatasi ya plastic huwa ni makubwa na hutokea mara kwa mara ukiliganisha na bwawa la udongo hivyo huathiri ukuaji na maisha ya samaki.
⤕Visima kwaajili ya kuhifadhia samaki wazazi na vifaranga wadogo:
Pia kuna visima maalum kwaajili ya kuhifadhia samaki wakubwa wazazi ama samaki wadogo (vifaranga).

No comments:
Post a Comment