MAMBO 5 MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA ULISHAJI
SAMAKI
Wewe kama mfugaji wa samaki ni mambo gani muhimu ya kuzingatia wakati
wa ulishaji wa chakula kwenye samaki, yafuatayo ni mambo muhimu yatakayo kukumbusha na
kukusaidia katika ulishaji samaki ili uweze kupata mavuno mazuri kwa samaki
wako.
➽Muda wa ulishaji,kuzingatia muda uliopangwa kulisha samaki wako ni jambo la msingi na lenye kuleta afya kwa ukuaji wa samaki,usilishe asubuhi sana kabla jua halijachomoza au kwa jioni baada ya jua kuzama au hali ya giza.
➽Pima kiwango/kipimo sahihi cha chakula kabla ya kuwapa samaki wako mfano kama samaki wanapaswa kula kilo moja hakikisha unapima kilo moja ndipo ulishe samaki wako.
➽Hakikisha unafahamu uzito wa samaki,kufahamu uzito wa samaki wako ni kitu muhimu cha kuzingatia kwani ndio kitakusaidia kufahamu unalisha kiasi gani samaki,kutofahamu uzito wa samaki wako kunaweza kupelekea kuwapa lishe ndogo au kubwa kitu ambacho kinaweza kupelekea hasara katika chakula na uchafukaji wa maji kwa haraka endapo umelisha kiwango cha chakula na kama chakula kitakuwa kidogo kitapelekea ukuaji hafifu kwa samaki.
➽Lisha sehemu moja au mbili kulingana na ukubwa wa bwawa lako,chagua upande mmoja ambao ndio utawazoesha samaki hapo ni vema ukalisha upande upepo unatokea ili kufanya chakula kisipotee na upepo na pia chakula ni rahisi kusogezwa na upepo kuelekea upande mwingine wa bwawa kirahisi.
➽Usilishe samaki wako wakati mvua inanyesha hata kama ni muda wa kulisha ndio huo,mfano mvua inanyesha saa nne na ndio muda sahihi wa kulisha samaki ni vema usilishe kabisa samaki wako.
Ulishaji bora wa samaki kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya uzalishaji wa samaki kwa kiwango kikubwa endapo utafuata taratibu na kanuni za kulisha samaki.
No comments:
Post a Comment