UFUGAJI WA KAA MATOPE
MUD CRAB FATTENING
Ufugaji huu wa kaa ni moja kati ya
ufugaji uliosahaulika Tanzania.Aina hii ya kaa hufugwa Zaidi na wakazi waishio
pembezoni mwa vyanzo vikubwa vya maji vya asili zaidi waishio pembezoni mwa
bahari.Kaa matope(mud crab) kwa asili hupenda eneo lenye matope hivyo hata
ufugaji wake hufanyika ndani ya eneo lenye mikoko pembezoni mwa bahari,kwa
kawaida eneo lenye miti ya mikoko aina ya udongo iliyotawala ni tope zito.
NJIA ZA UFUGAJI WA KAA MATOPE
>>Kwa kawaida kuna njia kuu mbili za
kienyeji zinazotumika kufugia kaa matope;
1) Njia ya kutenga vyumba kwa kutumia vipande vya mianzi/Vizimba vya mianzi(bamboo cages).
1) Njia ya kutenga vyumba kwa kutumia vipande vya mianzi/Vizimba vya mianzi(bamboo cages).
2) Njia ya kutenga bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi (Mud
crab bamboo pen culture).
*Pia faida nyingine kimazingira kaa
anasaidia sana kwenye ikolojia kama mvunjavuja vyakula kwaajili ya wenzake(decomposer), pia ujenzi wake unatumia Zaidi vitu vya asili yaani mianzi ambayo
inauwezo wa kuoza na kuisha hivyo haisababishi madhara kwenye viumbe wengine
majini ni tofauti na plastic material kama plastic net na mabomba ya plastic na
vinginevyo visivyoweza kuoza.
NJIA YA KUTENGA VYUMBA KWA KUTUMIA VIPANDE VYA MIANZI/VIZIMBA VYA MIANZI (BAMBOO CAGES)
Aina hii ya ufugaji mfugaji hupaswa
kutengeneza kizimba kikubwa na kukigawanya katika vyumba vidogo vidigo ambapo
ndipo watakapoishi kaa hao/Baadhi ya wafugaji huweka kaa moja mpaa wawili ndani
ya chumba kimoja.
Ukubwa wa kizimba kikubwa unaweza kuwa mkubwa kulingana na
uambuzi wa mfugaji na eneo alilo nalo japo urefu uwe kati ya m1.60 -
m1.83, lakini ukubwa wa vyumba ya ndani unatakiwa usivibane sana itawaathiri
katika ukuaji wao,kwa kawaida inatakiwa kwa kila chumba kimoja kiwe na urefu
usiopungua cm 92 na upana usiopungua cm23.Ufuniko wa juu unaacha na uwazi mdogo
kwaajili ya kulishia na kupata hewa ya kutosha(uwazi kati ya kipande cha mti
moja na mwingine).
MUONEKANO WA NJIA YA KUTENGA VYUMBA KWA KUTUMIA VIPANDE VYA MIANZI/VIZIMBA VYA
MIANZI (BAMBOO CAGES)
Baadhi ya faida za njia
ya vizimba ya kutenga vyumba ukilinganisha na bwawa la mianzi:
*Njia hii inapunguza ugombaniaji wa chakula na mahitaji mengine
kutokana na kwamba kila chumba kina idadi ndogo sana ya kaa.
*Lakini pia njia hii inapunguza uwezekano wa kaa kupigana,kupeana majeraha baina ya kaa wakubwa na
wadogo.
Udhaifu wake:
*Inatumia miti mingi kwenye ujenzi wake.
Njia ya kutenga bwawa maalumu la kutumia
vipande vya mianzi (Mud crab bamboo pen culture):
Hii ni njia rahisi
Zaidi,haitofautiani sana na njia iliyopita,utofauti wa njia hii ni kwamba
hakuna mgawanyo wa vyumba na mianzi
iliyojengewa pembezoni hujengwa katika mfumo wa kulalia ndani ya bwawa na si
kusimamisha wima,pia juu halifunikwe.Mianzi hulazwa kwa ulalo wa nyuzi 450.
Lengo la kulaza mianzi hii ni kuzuia
Kaa kupanda juu na kukimbia nje toka ndani ya bwawa,kutokana na uzito wa kaa na
utelezi wa mti wa aina ya mianzi kaa hawezi kupanda juu na kutoka nje kwenye
bwawa la aina hii.
Kwa kawaida kaa matope (mudcrab) ana
tabia ya kupendelea kutoroka nje ya kizimba ama bwawa kwaajili ya kwenda kutaga
kwenye kina kirefu kati ya mita 200,mazingira haya ndio yenye hali joto na chuvi
ya kiwango kizuri kwa ukuaji na upatikanaji wa chakula cha watoto wa kaa wakiwa
wadogo sana na zaidi na baadae wakifikia hatua ya vifaranga wanahama na kurudi
sehemu yenye tope na mchanganyiko wa maji chumvi na baridi (brackishwater
kwaajili ya ukuaji) hali hii ndio inayowafanya wawe wa kipekee na vigumu kwa
wao kufugwa na kuzalishwa majumbani (difficult tu breed and culture mudcrab in
captivity) ,pia hupendelea kutoka nje kwaajili ya kutafuta chakula(kaa anakula
mabaki ya vitu vingi kama mabaki ya samaki walio kufa,mollusca,chaza na
konokono bahari pamoja na mabaki ya maozea ya mimea ya majini,japokuwa kwa
wafugaji wa kienyeji huwalisha hata mabaki ya vyakula toka majumbani kama vile
ugali na vinginevyo kwani kaa huwa si mchaguzi sana wa vyakula).
Muonekano wa njia ya kutenga bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi
(Mud crab bamboo pen culture)
Baadhi ya Faida za Njia
ya kujenga bwawa maalumu la kutumia
vipande vya mianzi (Mud crab bamboo pond):
*Haitumii miti mingi hivyo ina faida kiuchumi na kimazingira
pia.
Udhaifu wake:
I *Inaruhusu kaa kupigana na kutoana majeraha wakati wa
kugombania chakula na kuwadhoofisha kaa wadogo kuwa anyone na kuathirika
kiukuaji.
Njia hizi mbili zote hufanyika eneo la ufukweni kwenye matope hasahasa chini ama pembezoni mwa miti aina ya mikoko eneo lenye maji kati ya mita 1 mpaka mita 2, eneo hili pia ndilo eneo lenye uwepo wa chakula kingi kwa kaa kwani ndilo eneo la mazalia ya samaki wengi na amaki wengi wadogo,konokono bahari,chaza na viumbe wengine hupatikana kwenye maeneo haya.
Faida za ufugaji wa Kaa matope
*Ni moja kati ya ufugaji wa kipekee
kutokana na changamoto ya kushindikana kuzalishwakwa njia za kisasa majumbani
hivyo huwafanya wafugaji wengi kuachana nao,hii inakupa faida kuwa na soko
Zaidi kutokana na kutokuwa na wazalishaji wengi.
*Lakini pia aina hii ya ufugaji ni
nzuri kwakuwa kaa endapo atalishwa vizuri na kuzingatia maelekkezo yote kaa
huwa anachukua mda mfupi kukuwa na kuwa tayari kwaajili ya kuuzwa ama kwa
matumizi,kwa kawaida kaa mdogo wa uzito kati ya grams 100 -175 ukamfuga anaweza kufikisha gram 250 – 350 kwa
muda wa siku 15 – 20 tu.
*Lakini faida nyingine ya aina hii ya
ufugaji haina gharama kubwa kwa upande wa chakula,kaa si mchaguzi sana wa
vyakula.
No comments:
Post a Comment