JIFUNZE KILIMO CHA MWANI KWA URAHISI NA LUGHA NYEPESI
(SEAWEED FARMING)
Mwani ni mmea wa baharini ,mmea huu kwa wasioufahamu unapatikana katika rangi tofauti tofauti ikiwemo kijani,nyekundu,brauni mpaka nyeusi.Mmea huu unaota maeneo ya karibia na fukwe za bahari (Kilimo hiki hufanyika Zanzibar na Mafia katika nchi yetu).
➧Hutumika kama chakula kwa binadamu na kwa viumbe waishio majini pia.
➧Mwani pia hutumika kutengenezea chachu za kutengenezea baadhi ya vyakula kama vile chocolate.
KILIMO CHA MWANI
Baadhi ya Mwani unaolimwa Tanzania;
➧Spinosum
➧Jamii ya Eucheuma cotonii
NJIA ZA ULIMAJI MWANI
Kuna njia kuu tatu yaani;
(1)Ya kutumia kamba (line method):
Njia hii unatakiwa kuwa na vipande vya miti(fito ndefu mbili zenye urefu sawa),baada ya hapo unachomeka miti hiyo sambamba kwa umbali wa 12M kutoka mti moja hadi mwingine.Unafunga kamba ya manila ambayo ni imara toka mti moja hadi mwingine.Baada ya hapo unafunga miche yako ya mwani katika kamba hiyo unaacha umbali mdogo kati ya mche moja na mwingine kama inavyoonekana(hakikisha miche inageukia upande sahihi wakati wa ufungaji usiigeuze).
(2) Kwa kutumia kichanya cha neti (Net method):
Hapa unatengeneza neti yenye vitundu vya ukubwa wa 60cm,mstatili huwa unaanzia ukubwa wa 2.5m kwa 5m ukubwa na umbo la neti yote,neti hiyo unaifunga kwenye vipande ya miti vinne ulivyo vichomeka majini,baada ya hapo unapandikiza miche yako kwa mtindo wa kuifunga kwenye neti yako eneo lote lililozunguukwa na vitundu vya neti:
(3)Njia ya tatu ni ya kutumia vipande vya mianzi vinavyoelea (Floating bamboo method):
Hapa unachotakiwa kufanya ni kuwa na vipande ya mianzi ya urefu wa 10m viwili na 12m viwili kwaajili ya umbo kubwa la nje (waweza ukawa na vipande vinginevyo vidogo kama utapenda kutenganisha vyuma vidogo katikati ya umbo au waweza bakia na umbo moja tu)baada ya hapo tafuta neti ya plastic isiyooza yenye vitundu kuanzia 60cm2 na upana na urefu unaoendana na umbo lako la mianzi ulilojenga kashi funga na kamba neti hiyo kwenye kona zote za umbo lako,hakikisha ina kaza na ni kamba isiyoooza mapema.Baada ya hapo tafuta mawe mazito ama vipande vya vyuma vine vifunge kwenye pembe zote za umbo kwa kutumia kamba ndefu na imara,hivi vitakusaidia kama nanga kuzuia shamba lako lisihamishwe na mawimbi ya maji,tafuta maboya ya plastic yanayoelea na ufunge kwenye kona hizohizo nne za umbo lako kubwa,hii itakusaidia shamba lako kuelea na kutokuzama chini(kienyeji na kwa urahisi tumia vipande ya mabox/makasha meupe yanayo fungia bidhaa kama redio na mengine,aina ile huwa haizami.
KANUNI ZA JUMLA KWA UCHAGUZI WA ENEO SAHIHI KWA AJILI YA KILIMO CHA AINA ZOTE ZA MWANI (SITE SELECTION FOR SEAWEED FARMING):
➽Chagua eneo lenye maji yaliyo kwenye mwendo kasi wa wastani ,usizidi sana waweza haribu shamba lako(water current speed should be 20m – 40m/second).
➽Eneo linatakiwa lisiwe katika muelekeo wenye upepo mkali sana wala mawimbi makali sana.
➽Epuka eneo ambako ni malango ya kuingia maji chumvi kwani itaathiri kiwango cha chumvi katika maji kwani mwani huwa hufanya vizuri kwenye maji chumvi mfano Eucheuma species hufanya vizuri kati ya kiwango cha chumvi cha 27 mpaka 30ppt.
➽Eneo liwe na hali joto kati ya 25c mpaka 30c (kwa maeneo mengi ya nchi yetu haina shida).
➽Kina cha maji kwenye shamba kinatakiwa kisiwe chini ya futi2 wakati maji yametoka na kisizidi futi 7 yakiwa yamejaa.
➽Hakikisha ardhi ya eneo husika ni imara kuweza kushikiza miti ya shamba lako.
➽Hakikisha eneo unalopanda mwani ni eneo ambalo aina hiyo ya mwani inaota,hakiki kwa kuangalia uwepo wa aina husika ya mwani.
No comments:
Post a Comment