MAMBO MUHIMU YA KUANGALIA WAKATI WA UCHAGUZI WA ENEO SAHIHI LA UCHIMBAJI WA BWAWA LA SAMAKI
Ni muhimu sana kuchagua eneo zuri ili kurahisisha na kufanikisha kwa urahisi kazi ya kufuga samaki kulingana na ukubwa wa eneo lako,si kila eneo la ardhi hufaa kwa ufugaji wa samaki.
Haya yafuatayo ni mambo muhimu sana ya kuangalia wakati wa kuchagua eneo zuri na sahihi la kuchimba bwawa la samaki:-
➽Eneo zuri la ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha na kuaminika kwa ufugaji wa samaki kwa kipindi kisicho pungua miezi 6 ambapo ndipo mavuno ya samaki huanza.
➽Udongo mzuri zaidi ni ule wa mfinyanzi ambao hutuamisha maji kirahisi ambao ujenzi wake ni nafuu,kama ardhi ni kichanga utalazimika kujenga kwa tofali au nailoni ngumu.
➽Eneo lisiwe na mteremko mkali sana,Kama upo uwe wastani ambao utafanya maji kutoka kirahisi,endapo eneo ni tambalale kabisa ni vema ukapata ushauri kutoka kwa mtaalam ili kufahamu namna bora ya kujenga bwawa kufanya maji yatoke kirahisi.
➽Eneo lisiwe katika mkondo wa maji au mavufuriko au maeneo ya mabondeni kwani ni hatari sana kwa shughuli za ufugaji kutapelekea samaki kusombwa na maji yatakayofurika kwenye bwawa na hivyo kuleta hasara katika mradi.
➽Ni vema eneo liwe karibu na nyumba ili kuthibiti wezi na maadui wa samaki,pia huwezesha kutoka huduma kwa urahisi.
Ukizingatia mambo haya kabla ya kuchimba bwawa la samaki utaepukana na hasara kubwa kwani wafugaji wengi wamekuwa wakikosea juu ya ujenga wa bwawa la samaki, ufugaji wa samaki unahitaji mazingira bora ili uweze kufanikiwa na kupata mavuno mazuri.
@Article By Musa Ngametwa
No comments:
Post a Comment