Wednesday 27 February 2019

CHAKULA CHA SAMAKI

CHAKULA CHA SAMAKI NA ULISHAJI WAKE

         
   Kuna aina mbalimbali ya vyakula vya samaki vinavyotengenezwa kwa mchanganyiko wa vitu mbalimbali vyenye virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika na samaki husika kulingana na umri wake na aina yake.

   Mfano: Chakula cha wazazi na watoto huwa na kiwango kikubwa cha protini ili kuwasaidia wazae watoto wengi ndani ya wakati, lakini  pia kuwasaidia watoto waweze kukua kwa haraka na ufasaha.

Kwa utaalamu vyakula hivi hutokana na mchanganyiko wa vitu kama:

Maharage, dagaa,pumba za mpunga na za mahindi, mtama,vitamin mix,madini na vingine vingi ambavyo husagwa na kuchanganywa kwa pamoja kwa kiwango maalumu kilingana na aina ya samaki anayeenda kulisha pia na umri wake. 

Baada ya hapo chakula hiki kama ni cha samaki wa kubwa ama vifaranga wakubwa kidogo basi kitatengenezwa kuwa katika mfumo wa tambi inayoelea na kuanikwa vizuri kwenye kivuli ili kikauke.

Kama ni cha watoto wadogo basi kiache katika mfumo wa poda tu. Kikisha kauka kabisa kihifadhi kwenye mifuko maalumu ili kisiharibike.

   Muhimu:Usianike chakula kwenye jua utapoteza virutubisho.


UHIFADHI WA CHAKULA CHA SAMAKI

Baadhi ya njia na mazingira ambayo unayoweza kuhifadhi chakula cha samaki: 

➧Baada ya kutengeneza chakula hifadhi kwenye vifuko vidogo maalumu.

➧Tengeneza kichanja kidogo chenye urefu wa nusu mita na tandika vifuko hivyo vyenye chakula           juu ya kichanja.

➧Kichanja kiwe ndani ya chumba chenye kuruhusu mzunguko wakutosha wa hewa safi ili kuepuka      chakula chako kisiharibiwe na bakteria wanaozaliana kwenye joto na unyevunyevu.

➧Kama una chakula kingi sana kichanja chaweza kuwa kwenye ghorofa zaidi moja au mbili, la            msingi ni kuacha nafasi ya kutosha kati ya ghorofa moja na ingine ili kuruhusu hewa yakutosha          kupita.
  
                   
 JINSI YA KULISHA SAMAKI NA MDA SAHIHI WA KULISHA SAMAKI

  Watu wengi hukosea mda sahihi wa kulisha samaki na hivyo kuathiri afya na ukuaji wa samaki kiujumla. Je ni muda gani sahihi wa kulisha samaki chakula?

 ➧Kitaalamu inashauriwa ulishe samaki wako asubuhi kati ya saa kumi na mbili mapaka saa moja na nusu na kwa muda wa jioni kati ya saa kumi na moja na nusu mpaka saa kumi na mbili na nusu.

Mda huu unapendekezwa kwa sababu kunakuwa hamna joto kali sana, wakati wa joto sana hasa mda kama wa mchana shughuli za ndani ya mwili huongezeka pia, samaki upoteza hamu ya kula hivyo haishauriwi kulisha mda huo.

Jinsi ya kulisha samaki

➧Kitaaalamu samaki hupaswi kumlisha kwa makadirio, inatakiwa uchukue sampuli ndogo ya    samaki toka kwenye bwawa lako halafu uwapime uzito na urefu, pia ujue ukubwa wa bwawa lako.
    
➧Kienyeji hasa kwa wakulima wadogo,unaweza kukadiria kwa kupima kiganja chako na                  kuwatupia kwenye bwawa.

 Zingatia: Tumia eneo moja tu la kuwalisha samaki wako kila siku,kama umeamua kuchagua  kona moja ya bwawa hakikisha unatumia hiyo kila siku.

    Uhifadhi mzuri wa chakula cha samaki na ulishaji bora wa samaki kwa kuzingatia kanuni kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya uzalishaji wa samaki kwa kiwango kikubwa endapo utafuata taratibu na kanuni za kulisha samaki na uchaguzi mzuri wa  chakula bora cha samaki.


No comments:

Post a Comment