Sunday, 20 January 2019

COMMON FISH SPECIES CULTURED IN TANZANIA

AINA ZA SAMAKI WAFUGWAO KWA WINGI TANZANIA

Tanzania samaki wanaofugwa wamegawanyika katika makundi mawili;



  ➤Kundi la kwanza ni wale wanaofugwa kwenye maji baridi/maji yasiyo ya chumvi,mfano Ziwa,kisima au bomba.



      ➤Kundi la Pili maji ya chumvi/bahari.





Maji ya Baridi/yasiyo na Chumvi


Baadhi ya aina ya samaki wanaopatikana kwenye kundi hili;


 i)Perege na Sato(Tilapia) Hii ni moja ya jamii ya samaki anayefugika kirahisi na kustahimili mazingira yeyote yale,japo samaki hawa wapo jamii nyingi duniani lakini kwa Tanzania jamii nzuri wa aina hiyo ya perege anatambulika kama Nile Tilapia Oreochromis Niloticus hii ndio aina Nzuri zaidi katika ufugaji wa samaki ambao kwa wastani wa miezi sita mpaka nane hufikisha gramu 250-400 kutegemea pia na aina ya ufugaji ni vema kushauriana na mtaalam wako kabla ya kufanya manunuzi ya mbegu ili kuepuka uchanganyaji wa mbegu nyingine zinazofanana na hao.



                          

                                             Sato (Tilapia)


 ii)Kambale (Catfish) Hii ni aina ya samaki ambao wanauwezo mkubwa zaidi wa kuvumilia mazingira kuliko perege,zipo aina nyingi sana kambale lakini aina bora na nzuri zaidi ni aina ya KOMBATI/mabaka mabaka,wastani wa ukuaji wake ni gramu 500 mpaka kilo moja kwa muda wa miezi sita kulingana pia na aina ya ufugaji.

                              

                                                      Kambale(Catfish)

Hizo ndio aina kuu mbili zinazofugwa hapa nchini kuzingatia sifa ya uvumilivu wa kimazingira,ukuaji na masoko.


Maji ya chumvi/Bahari

Samaki hawa hufugwa zaidi kwenye maeneo yaliyo karibu na BAHARI Kama vile Zanzibar,mtwara,lindi,pwani,na Tanga.

 i)Mwatiko (milk fish) Hii ni moja ya samaki wanaofugwa kwa Wingi zaidi kwenye maji ya bahari,wanauwezo kuvumilia mazingira na ukuaji mzuri,upakatikanaji wa mbegu zake mara nyingi hutegemea zaidi kuvua kando kando ya pwani ya miti ya mikoko,japo taasisi kadhaa zinafanya jitahada za kuzalisha samaki hawa kwa njia ya kitaalamu.

                   
                              

                                          Mwatiko(Milk Fish)


   ii) KAA (MudCrub) Kuna aina nyingi sana KAA lakini KAA GOGO ni aina nzuri kwa ukuaji,hawa mara nyingi hawafugwi kwenye mabwawa kama ilivyo samaki wengine,ufugaji wa samaki huyu hufugwa kwenye vizimba ambapo kila kizimba kimoja hukaa kaa mmoja,ni samaki wenye soko kubwa sana hasa kwenye hoteli za kitalii.

                      

                                                 Kaa (MudCrub)

   iii) Kamba (Prawns) hii ni moja ya jamii nyingine za samaki wa maji chumvi ambao hufugwa zaidi katika wilaya ya Mafia,bagamoyo na Zanzibar,Soko la samaki hawa ni kubwa na uhakika Zaidi,japo ufugaji wake unahitaji usimamizi wa karibu wa kitaalamu.Hivyo mfugaji anapaswa kujua anapaswa kafuga samaki aina gani kulingana na mazingira yake.




@Article by Musa Ngametwa
     

No comments:

Post a Comment