VIUMBE WAHARIBIFU NA MAGONJWA YA SAMAKI NA JINSI YA KUEPUKANANAYO
Viumbe wa haribifu kwenye bwawa la samaki si wengi sana japo kuna malalamiko bado yanayojitokeza toka kwa wafugaji.
Viumbe kama chura, Ndege, Kenge, Kicheche na wengineo wamekuwa wakiripotiwa kuingia marakawamara kwenye mabwawa na kula samaki.
Zifuatazo ni mbinu rahisi za kufanya ili kuepukana na tatizo hilo;
UDHIBITI WA VIUMBE WA ARDHINI KAMA CHURA KENGE, NYOKA NA WENGINEO
- Unapotengeneza bwawa lako hakikisha unachimba mfereji wa kina kidogo kwenda chini kuzunguka bwawa lako lote , mfereji huo tandika karatasi ya nailoni ili kuzuia upotevu wa sumu ya ya maji kama unatumia sumu ya maji na kwa anayetumia ya unga kuna haja ya kutandika karatasi hiyo ili kuepusha uharibifu wa mazingira( kemikali zisizohitajika ardhini).
- Umbali toka kwenye bwawa hadi kwenye mfereji angalau uwe 1m kutoka kwenye bwawa ili kutoruhusu mdudu amakiumbe chochote cha ardhini kuvuka mpaka wako kisha jaza maji yenye sumu ama sumu ya unga.
UDHIBITI WA VIUMBE WA ANGANI HASAHASA NDEGE
Tengeneza fremu ya mabanzi yenye ukubwa uliozidi bwawa lako kidogo litakaloweza kufunika eneo lote kuzunguka bwawa lako kisha tumia nyavu yenye matundu madogo kama zile zinazotumika kutengeneza madirisha ya nyumba lakini haikikisha matirio yake ni nailoni inayotumika kwenye uvuvi ili kuongezea uimara isioze mapema kisha wamba nyavu hiyo juu ya fremu yako na igongee kwenye kingo za fremu yako ya mabanzi kisha funika juu ya bwawa lako, hii itatumika kama ufuniko mda wote ili kuzuia viumbe wa angani waharibifu kama vile ndege kushindwa kuingia wala kuchukua samaki kwenye bwawa lako wakati wote.
MAGONJWA SHAMBULIZI KWA SAMAKI NA NJIA ZA KUEPUKANA NAYO
Moja kati ya mifugo isiyoshambuliwa sana na magonjwa ni samaki,lakini pia ni moja kati ya viumbe wanaoweza kuambukizana magonnjwa kwa urahisi endapo moja akiathirika na magonjwa na hatua za kumnusuru zisipochukuliwa mapema.Malalamiko mengi toka kwa wafugaji ni juu ya fungus,samaki hushambuliwa na fungus hasa kwa samaki wadogo kwa mfano kambale wakati wakuzalisha kwa njia ya kisasa kwa maana utalazimika kuweka mayai na kuacha vifaranga kwa wiki chache kwenye eneo dogo ili kuwatengenezea mazingira bandia yanayoendana na mazingira asili ili wazaliane(mfano unaweza kufanyia kwenye aquarium yenye kichanja,taa ya joto kwaajili ya kuzaliana),kwa muda huwa mara baada tu ya mayai kuanza kuanguliwa huwa wanaendelea kula kiini cha yai kwa siku chache za mwanzoni bila kutumia chakula kingine na baadaye atermia kabla ya kuwatoa na kuanza kuwapa chakula cha kawaida,kipindi hiki upo uwezekano mkubwa sana wa fungus kuzaliana kwa wingi na kushambulia samaki kutokana na uwepo wa viini(yolk) na maganda ya mayai ndani ya maji hivyo kupelekea maji kuwa machafu,eneo pia ni dogo,huleta ongezeko la joto,ukiunganisha na uchafu wa taka mwili za samaki hutengeneza mazingira mazuri kwa fungus na bacteria kuzaliana kwa wingi ndani ya maji na kushambulia samaki (mara nyingi huathiri idadi kubwa ya vifaranga wanaoanguliwa kisasa ndani ya aquarium na kuwasababishia vifo maana huambukizana kiurahisi kutakana na maji hutumika kama kisafirishi cha ugonjwa), hili huleta malalamiko mengi toka kwa wafugaji samaki wengi hudai kwanini wakifanya uzalishaji wa kitaalamu kwa kambale huzalisha samaki wengi sana lakini hawakui wote na wengi wanakufa katika hatua hii ya utoto?
Jibu ni hilo na pia yatupasa kukumbuka kuwa kinga ya mwili dhidi ya magojwa kwa viumbe wadogo ni ndogo haiwezi kulingana na viumbe wakubwa,hivyo inahitajika umakini sana wakuwa karibu na samaki wako hasa wakiwa katika hatua hii ya utoto,zingatia sana usafi wa maji,joto,kiwango cha kemikali ndani(acid na base) na ulishaji,ukiwa makini na hivi hakika utafurahia ukuaji wa samaki wako wote.
Kwa samaki wakubwa vivyohivyo huathiriwa na fungus japo ni kesi chache sana hutokea kwa samaki wakubwa ambazo kwa sehemu kubwa husababishwa na uzembe wa kuto kuzingatia usafi wa maji ndani ya bwawa.
NJIA ZA KUFANYA ILI KUEPUSHA TATIZO HILI
Hakikisha unabadilisha maji ndani ya wakati
maalum,pima usafi wa maji mara kwa mara kwa kutumia search disc ukigundua
yameanza kubadilika rangi sana na huioni vizuri ndani ya nusu mita jua maji ni
machafu na badilisha.
Lakini vile vile si uchafu wa maji kwa
kuonekana kwa macho tu,pia unatakiwa uwe umejijengea tabia ya kupima hali ya
kikemikali ya maji mara kwa mara(yaani kiwango cha acid,base,chumvi,joto)hivi
huweza kubadili hali joto ya maji,kuongeza sumu kama ammonia(kutokana na uchafu
kama kinyesi toka kwa samaki) na kutengeneza mazingira mazuri kwa vijidudu kama
bacteria kuzaliana kwa kasi na magonjwa ya ngozi kama fungus na mengine
kuongezeka na kushambulia samaki wako.
DALILI ZA MAGONJWA HAYO NI KAMA ZIFUATAZO
⧫Samaki kubadilika rangi ya ngozi
⧫Samaki kutoona vizuri na macho kuwa na ukungu
⧫Samaki kujawa na uteute uliopitiliza juu ya
ngozi yake.
⧫Samaki kukatikakatika baadhi ya viungo vyake
kama mikia
⧫Samaki kubabukababuka ama kuchubuka ngozi
⧫Samaki kujitenga na kuwa katika hali dhoofu.
Hizi ni baadhi ya dalili kuu ziko nyingine
nyingi.....
NINI KIFANYIKE UKIGUNDUA HALI KAMA HII
⧫Mtenge haraka samaki uliye muona na dalili
hizo ili asiwaambukize wenzake(mtoe na muweke kwenye bwawa ama chombo cha
pekeyake.
⧫Badilisha maji kwenye bwawa hilo na lifanyie
usafi wa uhakika bwawa lako,ikiwezekana tumia lime ama dawa nyinginezo salama
baada ya kutoa hayo maji na wakati wakufanyia usafi bwawa lako.
⧫Kwa samaki huyo uliyemtenga unaweza ukawa
unaendelea kumtibia taratibu akiwa katika sehemu tengefu isiyochangamana na
wenzake.
⧫Kwa njia nafuu na za kienyeji kama wewe ni
mkulima mdogo unaweza tumia maji ya chumvi kama ni magonjwa ya ngozi kwa
kumdumbukiza kwa dakika chache kila siku mpaka utakaapoona amepona vizuri.
⧫Usimchanganye na samaki wengine mara tu baada
ya kupona,muache kwa muda hata mwezi mzima kwakuwa magonjwa kama fungus
yanatabia yakuingia mpaka ndani kwenye damu hivyo yaweza kukudanganya kwa nje
kuwa amepona kumbe ndani bado anaugonjwa na kukusababishia hasara ya samakiwako
wote.
No comments:
Post a Comment