Saturday, 3 April 2021

 

MISITU YA MIKOKO NA IKOLOJIA YA VIUMBE BAHARI:


  • Je unaelewa nini kuhusu misitu ya mikoko? (Tujifunze pamoja)

Misitu ya mikoko ni misitu isiyopukutisha majani kimsimu(evergreen forests)inayopatikana katika ukanda wa mwambao katika eneo la bamvua kubwa na dogo(high and low tides)yenye uwezo wa kuhimili na kukua katika mazingira ya maji ya chumvi.

Ø  Misitu hii hustawi vizuri katika maeneo ya maingilio mito inapokutana na bahari.Ndani ya misitu ya mikoko kuna aina mbalimbali za mimea ,wanyama na wadudu.

 

Ø  Mfumo wa mikoko (Mangrove ecosystem) unahusisha eneo kati ya usawa wa maji ya bahari  wakati wa maji mafu,na usawa wa maji bahari wakati wa bamvua kuu,eneo ambalo lina maji,udongo,miti,wanyama pamoja na viumbe vingine vidogovodogo.

 

 

 

AINA ZA MIKOKO:

v  Kunaaina zipatazo zaidi ya 75 za mikoko ulimwenguni kote,hata hivyo katika nchi zetu za Afrilka Mashariki tuna takrini aina 8 za mikoko ambazo ni:

  1.        Mkandaa(Ceriops tagal)
  2. .       Msinzi (Bruguiera gymnorhiza)
  3. .       Msikudazi au Mkingu (Heritiera Littoralis)
  4. .       Mpia (Sonneratia alba)
  5. .       Mkaka au Mkoko(Rhizophora mucronata)
  6. .       Mkomafi (Xylocarpus granatum)
  7. .       Mchu(Avicennia marina)
  8. .       Mkandaa dume(Lumnitizera racemosa)

 

Ø  Kwanini mikoko inaweza kustawi kwenye maji ya chumvi?

Jibu rahisi: Miti ya mikoko inaweza kustawi katika eneo lenye maji ya chumvi tofauti na miti mingine kwakuwa ina maumbile ya kipekee yanayoiwezesha kupambana na hali hiyo ngumu ambayo kwa mimea mingine ingekufa

 

UMUHIMU WA KUHIFADHI NA KUTUNZA MISITU YA MIKOKO:

Umuhimu wa faida za mikoko unaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani

Faida zinazotokana na mazao ya misitu faida za moja kwamoja na faida za kimazingira zisizo za moja kwa moja;

  1. Nguzo za mikoko kwaajili ya ujenzi wa nyumba
  2. Ngozo za mikoko kwaajili ya biashara
  3. Mbao kwaajili ya samani na ujenzi wa vyombo vya usafiri wa majini(Mashua na majahazi)
  4. Magogo kwa kuchongea mitumbwi,mzinga ya nyuki ,vinu n.k
  5. Kuni
  6. Matunda na majani kwaajili ya dawa
  7. Majani kulisha mifugo (Mbuzi)

 

 

FAIDA ZISIZO ZA MOJA KWA MOJA (FAIDA ZA KIMAZINGIRA):

  1. Mikoko huzalisha na kuzunguusha virutubisho,hivyo hutumika kama chanzo cha chakula kwa mimea na wanyamayakiwemo matumbawe na majani bahari ambayo ni muhimu sana kwa upatikanaji wa samaki.
  2. Mikoko hukinga fukwe za bahari na mito dhidi ya momonyoko wa udongo unaosababishwa na mawimbi.
  3. 3.       Kupunguza kasi ya upepo na hivyo kuzuia au kupunguza vimbunga. 
  4. 4.       Kutumika kama chujio la kupunguza kasi ya udongo unaotoka juu unaoletwa na maji ya mito na mvua na hivyo kuzuia matumbawe na majani ya bahari yasifunikwe na tope jambo ambalo lingesababisha yafe. 
  5. 5.       Hupunguza nguvu ya sumu ya mabaki ya viwandani yanayotupwa baharini.
  6. 6.       Kutumika kama mojawapo ya vivutio kwa watalii
  7. 7.       Kutumika kama mojawapo ya maeneo muhimu ya utalii na mafunzo
  8. 8.       Maeneo muhimu ya matambiko(kwa kibibi/shamba la bibi)  
  9. 9.       Mikoko ni sehemu muhimu ya kuzaliana,kulishia na kulelea aina mbali mbali za samaki,hivyo kuwepo kwa misitu ya mikoko ni muhimu kwa maendeleo ya kazi za uvuvi.
  10.  10.   Ndani ya misitu ya mikoko hupatikana aina mbalimbali za wa nyama kama vile mbega,kima,tumbili,nguruwe,viboko n.k.
  11. 11.   Wavuvi hupata chambo cha kuvulia samaki ndani ya mikoko
  12. 12.   Mikoko hutumika kutengenezea mitego ya samaki pamoja na maboya kwaajili ya uvuvi

 

 

No comments:

Post a Comment