Thursday, 31 January 2019

JIPATIE BIDHAA MPYA KUTOKA A.A.S TANZANIA

        AAS DAGAA !!!!! (AAS SARDINES)⧫







AAS sardines ni bidhaa yetu mpya ya dagaa wa ziwani na walioandaliwa kwa kuzingatia afya na viungo asili,dagaa wetu wamekaangwa na viungo vifuatavyo:-

                                                       Limao
                                ⇝Chumvi
                                ⇝Tangawizi
                                ⇝Kitunguu saumu
Bei zetu:-
   ⇝2300/= Kwa bei ya Jumla
   ⇝2500/= Kwa bei ya Reja Reja




UKIVUTIWA NA BIDHAA WASILIANA NASI UWEZE KUWEKA ODA YAKO.
PIA TUNAHITAJI WAKALA WENGI KWA MIKOA IFUATAYO:

KILIMANJARO,ARUSHA,MBEYA,IRINGA,DODOMA,MOROGORO, SINGIDA, SHINYANGA, TANGA NA DAR ES SALAAM WASILIANA NASI KUPITIA NAMBA ZETU ZA SIMU AU KWA KUTUMIA EMAIL YETU:-

                                          Namba za Simu:

                              +255 764 175 381

                              +255 755 168 998

                                       Email:
                                                                                               aaservicetanzania@gmail.com

     ⟾KARIBUNI SANA⟽

BIDHAA MPYA KUTOKA A. A. S TANZANIA

   AAS sardines ni bidhaa yetu mpya ya dagaa wa ziwani walioandaliwa kwa kuzingatia afya na viungo asili,dagaa wetu wamekaangwa na viungo vifuatavyo:  
                         ⇝Tangawizi
                         ⇝Limao
                         ⇝Chumvi 

                         ⟿Kitunguu Saumu

             MUONEKANO WA BIDHAA YETU:-



BAADHI YA FAIDA ZA KIAFYA ZA DAGAAA NA VIUNGO VILIVYOTUMIKA KUANDAA DAGAA WA AAS: 

FAIDA KWA AFYA YA MOYO:

  Kama ilivyo kwa karanga na korosho,dagaa nao wameonesha kuwa na faida kubwa kwa wenye matatizo ya magonjwaya moyo. Dagaa wana virutubisho vingi na miongoni mwa virutubisho hivyo kunakiwango kikikubwa cha Omega-3 Fatty

Acids (EPA & DHA)
Katika tafiti nyingi za magonjwa ya moyo na tiba zake, virutubisho vya Omega 3 vimeonekana kuwa dawa au kinga kubwa sana ya magonjwa ya moyo. Chanzo kikuu cha virutubisho hivyo si vingine bali ni samaki pamoja na dagaa.

Aidha, dagaa pia ni chanzo kizuri cha Vitamin B12, ikiwa ni chanzo kizuri cha pili baada ya maini. Vitamin hii hufanyakazi kubwa ya kuboresha ustawi wa moyo na hivyo kuwa chakula kizuri cha kumpa ahueni au kinga madhubuti mlaji dhidi ya magonjwa ya moyo.

AFYA YA MIFUPA 

    Dagaa ni chanzo kingine kizuri cha madini ya Calcium' yenye jukumu la kuimarisha mifupa ya mwili, lakini pia kwenye dagaa kuna vitamin D ambayo huwa nadra sana kupatikana kwenye lishe.

Vitamin D hufanyakazi muhimu ya kuimarisha afya ya mifupa kwani ndiyo inayosaidia unyonywaji mwilini wa madini ya calcium'. Vile vile dagaa ni chanzo kizuri cha madini aina ya phosphorus',ambayo nayo huimarisha mifupa.

DAGAA NA MARADHI YA KANSA 

    Kwa miaka mingi, watafiti wameona jinsi ambavyo dagaa inavyoweza kudhibiti seli zinazosambaza saratani mwilini. Hivyo imethibitika pasi na shaka kuwa virutubisho vilivyomo kwenye dagaa huweza kutoa kinga kubwa dhidi ya ugonjwa wa saratani.


WAMEJAA PROTINI

   Kama una upungufu wa protini mwilini,basi kula dagaa kwani wao wana kiwango kikubwa cha kirutubisho hicho.Protini husaidia uzalishaji wa Amino acids' ambazo ni muhimu kwa uzalishaji wa chembe hai mwilini na uimarishaji wa mfumo wa kinga ya mwili (body immune system). 

Hizi ni baadhi tu ya faida zake na nyingine nyingi ambazo hazikuainishwa zipatikanazo kwenye viungo vilivyotumika kama tangawizi,vitunguu saumu na limao. 

TAHADHARI:

  Wagonjwa wa figo na wale wenye matatizo ya ;gout', wanashauriwa kula dagaa kiasi kidogo na kwa tahadhari kubwa au kuepuka kabisa. Sababu inayotolewa ni kwamba, kama ilivyo kwa baadhi ya vyakula vingine, dagaa huwa na vitu (purine) ambavyo vinaweza kuwasumbua watu wenye magonjwa hayo, vinginevyo dagaa siyo chakula cha kukosa kula! 

Chanzo: M.Mkavu (Mtaalamu wa tiba lishe Tanzania)


Tuesday, 29 January 2019

KILIMO CHA MWANI

JIFUNZE KILIMO CHA MWANI KWA URAHISI NA LUGHA NYEPESI     

(SEAWEED FARMING)


  Mwani ni mmea wa baharini ,mmea huu kwa wasioufahamu unapatikana katika rangi tofauti tofauti ikiwemo kijani,nyekundu,brauni mpaka nyeusi.Mmea huu unaota maeneo ya karibia na fukwe za bahari (Kilimo hiki hufanyika Zanzibar na Mafia katika nchi yetu).



BAADHI YA MATUMIZI YA MWANI

   ➧Hutumika kama chakula kwa binadamu na kwa viumbe waishio majini pia. 

  ➧Mwani pia hutumika kutengenezea chachu za kutengenezea baadhi ya vyakula kama vile chocolate. 

KILIMO CHA MWANI

Baadhi ya Mwani unaolimwa Tanzania;

    ➧Spinosum

    ➧Jamii ya Eucheuma cotonii



NJIA ZA ULIMAJI MWANI

  Kuna njia kuu tatu yaani; 

(1)Ya kutumia kamba (line method): 

Njia hii unatakiwa kuwa na vipande vya miti(fito ndefu mbili zenye urefu sawa),baada ya hapo unachomeka miti hiyo sambamba kwa umbali wa 12M kutoka mti moja hadi mwingine.Unafunga kamba ya manila ambayo ni imara toka mti moja hadi mwingine.Baada ya hapo unafunga miche yako ya mwani katika kamba hiyo unaacha umbali mdogo kati ya mche moja na mwingine kama inavyoonekana(hakikisha miche inageukia upande sahihi wakati wa ufungaji usiigeuze).

                           



(2) Kwa kutumia kichanya cha neti (Net method): 

Hapa unatengeneza neti yenye vitundu vya ukubwa wa 60cm,mstatili huwa unaanzia ukubwa wa 2.5m kwa 5m ukubwa na umbo la neti yote,neti hiyo unaifunga kwenye vipande ya miti vinne ulivyo vichomeka majini,baada ya hapo unapandikiza miche yako kwa mtindo wa kuifunga kwenye neti yako eneo lote lililozunguukwa na vitundu vya neti:
         
                             


(3)Njia ya tatu ni ya kutumia vipande vya mianzi vinavyoelea (Floating bamboo method): 

Hapa unachotakiwa kufanya ni kuwa na vipande ya mianzi ya urefu wa 10m viwili na 12m viwili kwaajili ya umbo kubwa la nje (waweza ukawa na vipande vinginevyo vidogo kama utapenda kutenganisha vyuma vidogo katikati ya umbo au waweza bakia na umbo moja tu)baada ya hapo tafuta neti ya plastic isiyooza yenye vitundu kuanzia 60cm2 na upana na urefu unaoendana na umbo lako la mianzi ulilojenga kashi funga na kamba neti hiyo kwenye kona zote za umbo lako,hakikisha ina kaza na ni kamba isiyoooza mapema.Baada ya hapo tafuta mawe mazito ama vipande vya vyuma vine vifunge kwenye pembe zote za umbo kwa kutumia kamba ndefu na imara,hivi vitakusaidia kama nanga kuzuia shamba lako lisihamishwe na mawimbi ya maji,tafuta maboya ya plastic yanayoelea na ufunge kwenye kona hizohizo nne za umbo lako kubwa,hii itakusaidia shamba lako kuelea na kutokuzama chini(kienyeji na kwa urahisi tumia vipande ya mabox/makasha meupe yanayo fungia bidhaa kama redio na mengine,aina ile huwa haizami.

                           


KANUNI ZA JUMLA KWA UCHAGUZI WA ENEO SAHIHI KWA AJILI YA KILIMO CHA AINA ZOTE ZA MWANI (SITE SELECTION FOR SEAWEED FARMING): 


➽Chagua eneo lenye maji yaliyo kwenye mwendo kasi wa wastani ,usizidi sana waweza haribu shamba lako(water current speed should be 20m – 40m/second). 

➽Eneo linatakiwa lisiwe katika muelekeo wenye upepo mkali sana wala mawimbi makali sana. 

➽Epuka eneo ambako ni malango ya kuingia maji chumvi kwani itaathiri kiwango cha chumvi katika maji kwani mwani huwa hufanya vizuri kwenye maji chumvi mfano Eucheuma species hufanya vizuri kati ya kiwango cha chumvi cha 27 mpaka 30ppt. 

➽Eneo liwe na hali joto kati ya 25c mpaka 30c (kwa maeneo mengi ya nchi yetu haina shida). 

➽Kina cha maji kwenye shamba kinatakiwa kisiwe chini ya futi2 wakati maji yametoka na kisizidi futi 7 yakiwa yamejaa. 

➽Hakikisha ardhi ya eneo husika ni imara kuweza kushikiza miti ya shamba lako. 

➽Hakikisha eneo unalopanda mwani ni eneo ambalo aina hiyo ya mwani inaota,hakiki kwa kuangalia uwepo wa aina husika ya mwani. 



Wednesday, 23 January 2019

UCHAGUZI SAHIHI WA ENEO KWA AJILI YA UCHIMBAJI WA BWAWA LA SAMAKI

MAMBO MUHIMU YA KUANGALIA  WAKATI WA UCHAGUZI WA ENEO SAHIHI LA UCHIMBAJI WA BWAWA LA SAMAKI


   Ni muhimu sana kuchagua eneo zuri ili kurahisisha na kufanikisha kwa urahisi kazi ya kufuga samaki kulingana na ukubwa wa eneo lako,si kila eneo la ardhi hufaa kwa ufugaji wa samaki.



  Haya yafuatayo ni mambo muhimu sana ya kuangalia wakati wa kuchagua eneo zuri na sahihi la kuchimba bwawa la samaki:-


Eneo zuri la ufugaji wa samaki ni lenye maji ya kutosha na kuaminika kwa ufugaji wa samaki kwa kipindi kisicho pungua miezi 6 ambapo ndipo mavuno ya samaki huanza.

Udongo mzuri zaidi ni ule wa mfinyanzi ambao hutuamisha maji kirahisi ambao ujenzi wake ni nafuu,kama ardhi ni kichanga utalazimika kujenga kwa tofali au nailoni ngumu.

Eneo lisiwe na mteremko mkali sana,Kama upo uwe wastani ambao utafanya maji kutoka kirahisi,endapo eneo ni tambalale kabisa ni vema ukapata ushauri kutoka kwa mtaalam ili kufahamu namna bora ya kujenga bwawa kufanya maji yatoke kirahisi.

Eneo lisiwe katika mkondo wa maji au mavufuriko au maeneo ya mabondeni kwani ni hatari sana kwa shughuli za ufugaji kutapelekea samaki kusombwa na maji yatakayofurika kwenye bwawa na hivyo kuleta hasara katika mradi.

Ni vema eneo liwe karibu na nyumba ili kuthibiti wezi na maadui wa samaki,pia huwezesha kutoka huduma kwa urahisi.

    Ukizingatia mambo haya kabla ya kuchimba bwawa la samaki utaepukana na hasara kubwa kwani wafugaji wengi wamekuwa wakikosea juu ya ujenga wa bwawa la samaki, ufugaji wa samaki unahitaji mazingira bora ili uweze kufanikiwa na kupata mavuno mazuri.

  @Article By Musa Ngametwa

Tuesday, 22 January 2019

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA ULISHAJI SAMAKI

     MAMBO 5 MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA ULISHAJI

SAMAKI


   Wewe kama mfugaji wa samaki ni mambo gani muhimu ya kuzingatia wakati wa ulishaji wa chakula kwenye samaki, yafuatayo ni mambo muhimu yatakayo kukumbusha na kukusaidia katika ulishaji samaki ili uweze kupata mavuno mazuri kwa samaki wako.



➽Muda wa ulishaji,kuzingatia muda uliopangwa kulisha samaki wako ni jambo la msingi na lenye kuleta afya kwa ukuaji wa samaki,usilishe asubuhi sana kabla jua halijachomoza au kwa jioni baada ya jua kuzama au hali ya giza.



➽Pima kiwango/kipimo sahihi cha chakula kabla ya kuwapa samaki wako mfano kama samaki wanapaswa kula kilo moja hakikisha unapima kilo moja ndipo ulishe samaki wako.



➽Hakikisha unafahamu uzito wa samaki,kufahamu uzito wa samaki wako ni kitu muhimu cha kuzingatia kwani ndio kitakusaidia kufahamu unalisha kiasi gani samaki,kutofahamu uzito wa samaki wako kunaweza kupelekea kuwapa lishe ndogo au kubwa kitu ambacho kinaweza kupelekea hasara katika chakula na uchafukaji wa maji kwa haraka endapo umelisha kiwango cha chakula na kama chakula kitakuwa kidogo kitapelekea ukuaji hafifu kwa samaki.

➽Lisha sehemu moja au mbili kulingana na ukubwa wa bwawa lako,chagua upande mmoja ambao ndio utawazoesha samaki hapo ni vema ukalisha upande upepo unatokea ili kufanya chakula kisipotee na upepo na pia chakula ni rahisi kusogezwa na upepo kuelekea upande mwingine wa bwawa kirahisi.

Usilishe samaki wako wakati mvua inanyesha hata kama ni muda wa kulisha ndio huo,mfano mvua inanyesha saa nne na ndio muda sahihi wa kulisha samaki ni vema usilishe kabisa samaki wako.


  Ulishaji bora wa samaki kunaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya uzalishaji wa samaki kwa kiwango kikubwa endapo utafuata taratibu na kanuni za kulisha samaki.


@Article By Musa Ngametwa

Monday, 21 January 2019

MAMBO MUHIMU YANAVYOPELEKEA MAVUNO MAZURI YA SAMAKI

  MAMBO 7 MUHIMU YANAYOPELEKEA  MAVUNO MAZURI YA SAMAKI




   Kama mfugaji wa samaki unapaswa kuzingatia mambo haya muhimu ili uweze kupata faida na mavuno mazuri ya samaki:-
  
Uchaguzi sahihi wa mbegu za samaki, kutapelekea kuvuna samaki wakiwa na uzito sahihi ndani ya muda sahihi uliokusudiwa.

➽Kupandikiza samaki wako kwa idadi maalumu ndani ya bwawa lako, hii itapelekea samaki kukua vizuri kwa kuwa watapata nafasi na hewa ya kutosha ndani ya bwawa.

➽Kulisha chakula kilicho na virutubisho vizuri na vilivyo changanywa kwa uwiano kulingana na rika la samaki husika na aina ya samaki mwenyewe mfano kama ni samaki sato tengeneza chakula kutokana na jamii ya samaki hao usiwape samaki wengine,fuata kanuni bora za ukaushaji wa chakula na uhifadhi ili kisipoteze ubora wake.

➽Lisha samaki wako kwa wakati maalumu na ulioshauriwa na wataalamu ambapo kwa wastani wa mifumo mingi ya ufugaji ni asubuhi kuanzia saa 2 - 4 na jioni kuanzia saa 10-12 jioni, usilishe samaki wako asubuhi sana na jioni sana wakati jua limezama.

➽Lisha samaki wako chakula cha kutosha washibe
kiwango cha chakula wanachopaswa kupewa hutegemea na uzito wa samaki husika mfano samaki akiwa mdogo wastani wa gramu 20 atakula kidogo kulinganisha na samaki mwenye uzito wa gramu 200, ni muhimu sana kufahamu idadi ya samaki wako na uzito wao ili uwape chakula kutokana na vigezo muhimu vya uzito na idadi.

➽Badilisha maji kwa wakati pale tu unahisi yamechafuka, dalili za awali maji kuchafuka ni kuwa na rangi ya ukijani uliokolea na dalili nyingine maji kutoa harufu , hivyo unapaswa kufuata kanuni na taratibu za ubadilishaji wa maji.

➽Hakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwenye mradi ikiwemo kuweka wavu juu ya bwawa ili kuzuia ndege ,kenge na fisi maji (otters) au kwa lugha iliyozoeleka VICHECHE, kufanya hivi kutapelekea kuvuna samaki wako kwa idadi  ile ile ulio pandikiza awali ndani ya bwawa lako.

   Haya ndo mambo muhimu unayopaswa kujua ili uweze kufanikiwa katika ufugaji wa samaki ukizingatia haya na kanuni na taratibu zote nyingine za ufugaji kutapelekea mavuno mazuri ya samaki na kupata faida. 

@Article by Musa Ngametwa

  

Sunday, 20 January 2019

COMMON FISH SPECIES CULTURED IN TANZANIA

AINA ZA SAMAKI WAFUGWAO KWA WINGI TANZANIA

Tanzania samaki wanaofugwa wamegawanyika katika makundi mawili;



  ➤Kundi la kwanza ni wale wanaofugwa kwenye maji baridi/maji yasiyo ya chumvi,mfano Ziwa,kisima au bomba.



      ➤Kundi la Pili maji ya chumvi/bahari.





Maji ya Baridi/yasiyo na Chumvi


Baadhi ya aina ya samaki wanaopatikana kwenye kundi hili;


 i)Perege na Sato(Tilapia) Hii ni moja ya jamii ya samaki anayefugika kirahisi na kustahimili mazingira yeyote yale,japo samaki hawa wapo jamii nyingi duniani lakini kwa Tanzania jamii nzuri wa aina hiyo ya perege anatambulika kama Nile Tilapia Oreochromis Niloticus hii ndio aina Nzuri zaidi katika ufugaji wa samaki ambao kwa wastani wa miezi sita mpaka nane hufikisha gramu 250-400 kutegemea pia na aina ya ufugaji ni vema kushauriana na mtaalam wako kabla ya kufanya manunuzi ya mbegu ili kuepuka uchanganyaji wa mbegu nyingine zinazofanana na hao.



                          

                                             Sato (Tilapia)


 ii)Kambale (Catfish) Hii ni aina ya samaki ambao wanauwezo mkubwa zaidi wa kuvumilia mazingira kuliko perege,zipo aina nyingi sana kambale lakini aina bora na nzuri zaidi ni aina ya KOMBATI/mabaka mabaka,wastani wa ukuaji wake ni gramu 500 mpaka kilo moja kwa muda wa miezi sita kulingana pia na aina ya ufugaji.

                              

                                                      Kambale(Catfish)

Hizo ndio aina kuu mbili zinazofugwa hapa nchini kuzingatia sifa ya uvumilivu wa kimazingira,ukuaji na masoko.


Maji ya chumvi/Bahari

Samaki hawa hufugwa zaidi kwenye maeneo yaliyo karibu na BAHARI Kama vile Zanzibar,mtwara,lindi,pwani,na Tanga.

 i)Mwatiko (milk fish) Hii ni moja ya samaki wanaofugwa kwa Wingi zaidi kwenye maji ya bahari,wanauwezo kuvumilia mazingira na ukuaji mzuri,upakatikanaji wa mbegu zake mara nyingi hutegemea zaidi kuvua kando kando ya pwani ya miti ya mikoko,japo taasisi kadhaa zinafanya jitahada za kuzalisha samaki hawa kwa njia ya kitaalamu.

                   
                              

                                          Mwatiko(Milk Fish)


   ii) KAA (MudCrub) Kuna aina nyingi sana KAA lakini KAA GOGO ni aina nzuri kwa ukuaji,hawa mara nyingi hawafugwi kwenye mabwawa kama ilivyo samaki wengine,ufugaji wa samaki huyu hufugwa kwenye vizimba ambapo kila kizimba kimoja hukaa kaa mmoja,ni samaki wenye soko kubwa sana hasa kwenye hoteli za kitalii.

                      

                                                 Kaa (MudCrub)

   iii) Kamba (Prawns) hii ni moja ya jamii nyingine za samaki wa maji chumvi ambao hufugwa zaidi katika wilaya ya Mafia,bagamoyo na Zanzibar,Soko la samaki hawa ni kubwa na uhakika Zaidi,japo ufugaji wake unahitaji usimamizi wa karibu wa kitaalamu.Hivyo mfugaji anapaswa kujua anapaswa kafuga samaki aina gani kulingana na mazingira yake.




@Article by Musa Ngametwa
     

Sunday, 13 January 2019

UFUGAJI WA KAA MATOPE KWA KUTUMIA NJIA ZA ASILI AU KIENYEJI

 UFUGAJI WA KAA MATOPE

MUD CRAB FATTENING






  Ufugaji huu wa kaa ni moja kati ya ufugaji uliosahaulika Tanzania.Aina hii ya kaa hufugwa Zaidi na wakazi waishio pembezoni mwa vyanzo vikubwa vya maji vya asili zaidi waishio pembezoni mwa bahari.Kaa matope(mud crab) kwa asili hupenda eneo lenye matope hivyo hata ufugaji wake hufanyika ndani ya eneo lenye mikoko pembezoni mwa bahari,kwa kawaida eneo lenye miti ya mikoko aina ya udongo iliyotawala ni  tope zito.

 NJIA ZA UFUGAJI WA KAA MATOPE 
              
>>Kwa kawaida kuna njia kuu mbili za kienyeji                  zinazotumika   kufugia kaa matope;

      1) Njia ya kutenga vyumba kwa kutumia vipande vya mianzi/Vizimba vya mianzi(bamboo cages).

        2) Njia ya kutenga  bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi (Mud crab bamboo pen  culture). 
                                     

     NJIA YA KUTENGA VYUMBA KWA KUTUMIA VIPANDE VYA                             MIANZI/VIZIMBA VYA MIANZI                                          (BAMBOO CAGES)

  
   Aina hii ya ufugaji mfugaji hupaswa kutengeneza kizimba kikubwa na kukigawanya katika vyumba vidogo vidigo ambapo ndipo watakapoishi kaa hao/Baadhi ya wafugaji huweka kaa moja mpaa wawili ndani ya chumba kimoja.

  Ukubwa wa kizimba kikubwa unaweza kuwa mkubwa kulingana na uambuzi wa mfugaji na eneo alilo nalo japo urefu uwe kati ya m1.60 - m1.83, lakini ukubwa wa vyumba ya ndani unatakiwa usivibane sana itawaathiri katika ukuaji wao,kwa kawaida inatakiwa kwa kila chumba kimoja kiwe na urefu usiopungua cm 92 na upana usiopungua cm23.Ufuniko wa juu unaacha na uwazi mdogo kwaajili ya kulishia na kupata hewa ya kutosha(uwazi kati ya kipande cha mti moja na mwingine).
                                   

      MUONEKANO WA NJIA YA KUTENGA VYUMBA KWA KUTUMIA VIPANDE VYA  MIANZI/VIZIMBA VYA MIANZI          (BAMBOO CAGES)                    




        Baadhi ya faida za njia ya vizimba ya kutenga vyumba       ukilinganisha na bwawa la mianzi:


      *Njia hii inapunguza ugombaniaji wa chakula na mahitaji  mengine kutokana na kwamba kila chumba kina idadi ndogo  sana ya kaa.

      *Lakini pia njia hii inapunguza uwezekano wa kaa   kupigana,kupeana majeraha baina ya kaa wakubwa na
     wadogo.

                 Udhaifu wake:

        *Inatumia miti mingi kwenye ujenzi wake.


  Njia ya kutenga  bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi (Mud crab bamboo pen culture):

      Hii ni njia rahisi Zaidi,haitofautiani sana na njia iliyopita,utofauti wa njia hii ni kwamba hakuna mgawanyo wa vyumba   na mianzi iliyojengewa pembezoni hujengwa katika mfumo wa kulalia ndani ya bwawa na si kusimamisha wima,pia juu halifunikwe.Mianzi hulazwa kwa ulalo wa nyuzi 450.

      Lengo la kulaza mianzi hii ni kuzuia Kaa kupanda juu na kukimbia nje toka ndani ya bwawa,kutokana na uzito wa kaa na utelezi wa mti wa aina ya mianzi kaa hawezi kupanda juu na kutoka nje kwenye bwawa la aina hii.

     Kwa kawaida kaa matope (mudcrab) ana tabia ya kupendelea kutoroka nje ya kizimba ama bwawa kwaajili ya kwenda kutaga kwenye kina kirefu kati ya mita 200,mazingira haya ndio yenye hali joto na chuvi ya kiwango kizuri kwa ukuaji na upatikanaji wa chakula cha watoto wa kaa wakiwa wadogo sana na zaidi na baadae wakifikia hatua ya vifaranga wanahama na kurudi sehemu yenye tope na mchanganyiko wa maji chumvi na baridi (brackishwater kwaajili ya ukuaji) hali hii ndio inayowafanya wawe wa kipekee na vigumu kwa wao kufugwa na kuzalishwa majumbani (difficult tu breed and culture mudcrab in captivity) ,pia hupendelea kutoka nje kwaajili ya kutafuta chakula(kaa anakula mabaki ya vitu vingi kama mabaki ya samaki walio kufa,mollusca,chaza na konokono bahari pamoja na mabaki ya maozea ya mimea ya majini,japokuwa kwa wafugaji wa kienyeji huwalisha hata mabaki ya vyakula toka majumbani kama vile ugali na vinginevyo kwani kaa huwa si mchaguzi sana wa vyakula).


   Muonekano wa njia ya kutenga bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi 
          (Mud crab bamboo pen culture)







   Baadhi ya Faida za Njia ya kujenga  bwawa maalumu la kutumia vipande vya mianzi (Mud crab bamboo pond):
  
        *Haitumii miti mingi hivyo ina faida kiuchumi na kimazingira pia.

    Udhaifu wake: 
  
I   *Inaruhusu kaa kupigana na kutoana majeraha wakati wa kugombania chakula na kuwadhoofisha kaa wadogo kuwa anyone na kuathirika kiukuaji.
     Njia hizi mbili zote hufanyika eneo la ufukweni kwenye matope hasahasa chini ama pembezoni mwa miti aina ya mikoko eneo lenye maji kati ya mita 1 mpaka mita 2, eneo hili pia ndilo eneo lenye uwepo wa chakula kingi kwa kaa kwani ndilo eneo la mazalia ya samaki wengi na amaki wengi wadogo,konokono bahari,chaza na viumbe wengine  hupatikana kwenye maeneo haya.



                                      Faida za ufugaji wa Kaa matope

     *Ni moja kati ya ufugaji wa kipekee kutokana na changamoto ya kushindikana kuzalishwakwa njia za kisasa majumbani hivyo huwafanya wafugaji wengi kuachana nao,hii inakupa faida kuwa na soko Zaidi kutokana na kutokuwa na wazalishaji wengi.

      *Lakini pia aina hii ya ufugaji ni nzuri kwakuwa kaa endapo atalishwa vizuri na kuzingatia maelekkezo yote kaa huwa anachukua mda mfupi kukuwa na kuwa tayari kwaajili ya kuuzwa ama kwa matumizi,kwa kawaida kaa mdogo wa uzito kati ya grams 100 -175  ukamfuga anaweza kufikisha gram 250 – 350 kwa muda wa siku 15 – 20 tu.

     *Lakini faida nyingine ya aina hii ya ufugaji haina gharama kubwa kwa upande wa chakula,kaa si mchaguzi sana wa vyakula.

 *Pia faida nyingine kimazingira kaa anasaidia sana kwenye ikolojia kama mvunjavuja vyakula kwaajili ya wenzake(decomposer), pia ujenzi wake unatumia Zaidi vitu vya asili yaani mianzi ambayo inauwezo wa kuoza na kuisha hivyo haisababishi madhara kwenye viumbe wengine majini ni tofauti na plastic material kama plastic net na mabomba ya plastic na vinginevyo visivyoweza kuoza. 



Wednesday, 2 January 2019

UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA VIZIMBA

 UFUGAJI WA SAMAKI KWA KUTUMIA VIZIMBA

(FLOATING NET CAGE FISH FARMING)


    Hii ni aina ya ufugaji samaki kwa kutumia vizimba/cages.Vizimba hivi huwa vya maumbo tofauti tofauti kama mraba,mstatili na umbo la pipa.  

Ndani ya vizimba hivi ndimo samaki hufugwa,vizimba hutegwa majini eidha kwenye maziwa,mabwawa,baharini ama mtoni. Baada ya hapo samaki hufugwa humo mpaka wakati wa uvunaji.

Aina hii ya ufugaji pia kwa lugha ya kigeni inapofanyika kwenye vyanzo vya maji vya asili hujulikana kama off-shore cultivation/outdoor fish farming  ikifanyika  baharini.

             MUONEKANO WA UFUGAJI WA KUTUMIA VIZIMBA ZIWANI                               (FLOATING NET CAGE FISH FARMING) 

                           

Moja ya wataalamu wa ufugaji samaki kutoka AAS ndugu Donald Kusekwa Masondole akitembelea mradi na kushiriki zoezi la ulishaji samaki  na kutoa ushauri wa kitaalamu:
 
 
>>Faida za aina hii ya ufugaji hasa ukifanyika baharini,mitoni na maziwani:

   *Samaki hawawezi kupata mabadiliko ya joto mwilini kirahisi kwani eneo lenye maji(space) inakuwa ni kubwa hivyo hufanya uwepo wa hewa ya oxygen ya kutosha ndani ya kizimba,uwepo wa hali joto isiyo panda ghafla na kushuka kupita kiasi( extremely temperature fluctuation).

    *Uwepo wa chakula cha asili cha kutosha (Algae,Phyto  plankton,Zoo Plankton).

   *Pia uwepo wa maji mengi yaliyo kwenye mwendo kutokana na mawimbi ama mkondo husaidia sana  kwenye suala la uzalianaji kwa aina ya samaki wasio zaliana kwenye maji yaliyo simama(stagnant water).

Hivi vyote kwa pamoja hupelekea ukuaji wa samaki aneyefugwa kwa aina hii ya ufugaji kukua vizuri na kwa haraka kuliko yule anayefugwa kwenye bwawa.


>>Udhaifu wa njia hii ya ufugaji kwa mimea na viumbe  waishio baharini,mitoni na maziwani (Negative effect of Cage fish farming in the aquatic biodiversity):


    *Aina hii ya ufugaji yaweza kuwa hatari kimazingira endapo mfugaji hatakuwa makini yaweza kuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira ya majini,fukwe na viumbe waishio majini kwa ujumla,endapo  mfugaji hata kuwa makini katika suala la kuzingatia ubora/viwango vya vifaa alivyotumia kutengenezea cages zake ama kuzingatia muda sahihi wa kubadili vifaa hivyo na kuweka vipya.vitu kama nyavu za plastic na plastic materials nyingine anazotumia kwenye ufugaji vikiharibika ama kwa bahati mbaya kuingia majini huweza kuathiri maisha ya viumbe waishio kwenye vyanzo hivyo vya maji.

    * Pia Utumiaji wa kemikali katiki uzalishaji,ukuzaji na kutibu ama kinga si mzuri kufanya katika aina hii ya ufugaji,kemikali hizo huweza kuathiri viumbe na mimea wanaopatikana katika chanzo hicho cha maji na hata kukaribisha uwepo wa viumbe wapya na hatarishi kwa viumbe wa zamani.
 
>>Udhaifu wa kiuchumi(economic effect):


    *Pia aina hii ya ufugaji ni chaguzi (selective),ni rahisi zaidi kwa watu waishio pembezoni mwa vyanzo vikubwa  vya asili vya maji.

    *Lakini pia aina hii ya ufugaji unagharama kidogo Zaidi ya ule wa mabwawa kwa upande wa miundombinu yake.