Project ya kutoa elimu juu ya ufugaji bora wa samaki na ukulima bora wa mazao kwa lengo la kupunguza kiwango cha uvuvi haramu na uharibifu wa rasilimali zetu baharini,maziwani,mitoni na kwenye mbuga zetu za wanyama,tunatoa huduma zetu kwenye vikundi mbalimbali kwenye jamii ikiwemo wavuvi,wawindaji,wajasiria mali,wakulima,wafugaji na vijana.
Tunatoa huduma kwa njia ya kuendesha semina maeneo mbalimbali,kwenye kumbi mbalimbali na kwenye vyombo vya habari, pia tunasimamia miradi ya ujenzi wa mabwawa ya ufugaji samaki katika viwango sahihi.
Pia tunawaunganisha wafugaji na wazalishaji wa mbegu bora za samaki,wauzaji wa chakula na vifaa kwajili ya ufugaji na pia tunatoa ushauri juu ya ufugaji samaki na kilimo bora.
Unaweza kutupata kwenye ukurasa wetu wa facebook kwa jina hilohilo, Pia tunapatikana kwenye Youtube channel yetu kwa jina la AAS TANZANIA LTD pia kupitia kwenye blog yetu hii www.aaservicetanzania.blogspot.com ambapo tutakuwa tunarusha taarifa zetu na matukio mbalimbali tutakayofanya tukiwa tunawatembelea wakulima na wafugaji kwenye miradi yao na pia tutakapokuwa tunafanya semina sehemu mbalimbali.
Kwa mawasiliano/mualiko wa kuendesha semina n.k tupigie ama tuandikie kupitia:
+255(0) 764 175 381
+255(0) 755 168 998
aaservicetanzania@gmail.com