Thursday, 18 July 2019

UMUHIMU WA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI (KIENYEJI)

     KUKU WA ASILI(KIENYEJI)     


    Ufugaji wa kuku wa Asili ni jambo lisilo geni katika kaya zetu hapa nchini ni kuku wanaopendwa kufugwa na kuliwa na watu wengi kutokana na uasili wake. Ni dhahiri kwa sasa kuku wa asili(kienyeji) wamekuwa ghali na wanathamani kuliko kuku wa kisasa.

   Kuku hawa wa asili(kienyeji) kuna wanaofuga kwa minajili ya mayai,nyama ama kwa lengo la mradi wa biashara na kujipatia riziki zao.


Kuku wa Asili(kienyeji)

FAIDA NA CHANGAMOTO ZA UFUGAJI WA KUKU WA ASILI(KIENYEJI)


Ufugaji wa kuku wa asili unamanufaa mengi kwa mfano;kuku hutumia eneo dogo kuliko wanyama wengine wa kufugwa,pia hutumia chakula kidogo hivyo ufugaji unaweza kuendeshwa bila kutumia mtaji mkubwa.

  Hizi ni baadhi ya faida na changamoto za ufugaji wa kuku wa asili(kienyeji);

                          Faida za ufugaji wa kuku wa asili

  • Gharama nafuu za kuanzisha na kuendesha mradi wa kuku wa asili.
  • Chanzo cha kipato -mfugaji upata fedha akiuza kuku au mayai.
  • Chanzo cha ajira- ufugaji wa kuku hutoa ajira kwa jamii
  • Nyama ya kuku ni kitoweo kitamu kinachopendwa na kila mtu.
  • Kiini cha njano cha yai kinaweza kutumika kutengenezea mafuta ya nywele.
  • Kuku wa kienyeji anasaidia kusafisha mazingira kwa kula wadudu na kuongeza rutuba kwa mbolea inayotokana na kinyesi cha kuku ambacho hakina kemikali.
  • Mayai huweza kutumika kwa tiba
  • Manyoya yake huweza kutumika kwa mapambo
  • Tangu enzi jogoo amekuwa akitumika kutukumbusha muda/wakati hasa wakati wa alfajiri pale anapowika


               Changamoto za ufugaji wa kuku wa asili

  • Magonjwa kama mdondo na ndui huathiri ufugaji wa kuku.
  • Wezi,wanyama na ndege hushambulia kuku.
  • Ukosefu wa mabanda bora ya kuku
  • Ukuaji taratibu iwapo watakosa lishe nzuri
  • Ukosefu wa chanjo kwa wakati huweza kuathiri ukuaji wa kuku au kuku kupata magonjwa kwa haraka.

             Baadhi ya magonjwa yashambuliayo kuku wa asili;
  • Kideri/mdondo
  • Ndui ya kuku
  • Kipindukipindu cha kuku
  • Mafua ya kuku
  • Homa ya matumbo
  • Kuhara damu
  • Wadudu kama viroboti,chawa,utitiri, kupe wa kuku.

   Pamoja na sifa hizo na changamoto za ufugaji wa kuku wa asili ni muhimu kuku hao wakapewa matunzo mazuri wawekwe kwenye mabanda mazuri na imara, Pia wapewe maji na chakula cha kutosha pia kuwapa chanjo kwa wakati za kuzuia magonjwa mbalimbali...