Ndugu mfuatiliaji wa fululizo za masomo ya
AAS ufugaji wa samaki ni teknolojia inayokuwa kwa kasi sasa katika nchi yetu
pia yaweza kuwa ni njia moja wapo itakayosaidia katika juhudi za kutunza
mazingira,kukuza kipato na pia kuunga mkono juhudi za Raisi wetu wa awamu ya
Tano Dr. John Joseph Pombe Magufuli za kuelekea katika uchumi wa viwanda.
Leo
tutajifunza aina za ufugaji wa samaki kwa njia za kisasa na za gharama nafuu
pia zinazingatia uhifadhi wa mazingira (aina hii ya ufugaji ni rahisi hata kwa
Mtanzania mwenye eneo dogo,anayeishi katikati ya mji anaweza kufuga bila shida
yeyote):
UFUGAJI WA SAMAKI KWA
KUTUMIA MABWAWA TURBAI YA PLASTIC/MABWAWA YANAYO HAMISHIKA:
Aina hii ya ujenzi wa mabwawa hutengenezwa
kwa kutumia turbai maalumu za plastic pamoja na pomba za chuma zinazopindwa na
kutengenezwa kuwa katika umbo la mraba ama mstatili,mabomba haya huwa na ukubwa
tofauti ili yaweze kuvaana kirahisi na kutoa umbo la bwawa na kuchomolewa
kirahis wakati wakuhama ili kumrahisishia mfugaji kutokufungwa kufanya kazi
sehemu moja.Aina hii ya mabwawa ujenzi wake na ufungwaji wake wa mabomba unafanana
sana na ufungwaji wa mahema.
MUONEKANO WA BWAWA LA KUHAMISHIKA:
FAIDA ZA UJENZI HUU WA
MABWAWA:
Yana
gharama nafuu kwa upande wa ujenzi hivyo humsaidia mfugaji kutumia gharama
ndogo katika ujenzi.Hapa mfugaji hatakuwa na gharama za kununua
cement,nondo,kokoto,mchanga wala kutafuta mashine za kuchimba,anachotafuta ni
bomba za chuma na turbai nzito ya plastic basi.
Yanazingatia
uhifadhi wa mazingira,hapa mfugaji hatachimba ardhi kwani yenyewe huanzia juu
ya uso wa ardhi,pia kama ni mfugaji anayetumia kemikali katika ufugaji wake
kwenye chakula ama kutibu samaki basi aina hii ya mabwawa inakinga kemikali
zile kudhuru ardhi na viumbe wengine waishio arhini (Angalizo ili kutimiza hili
pindi tu mfugaji anapoona plastic sheet imechakaa na anataka kubadii nyingine
anapaswa kuzingatia sana utupaji wa mifuko hiyo sehemu sahihi na si kuiacha
izagae ovyo,ni mbaya kwenye mazingira,ni vyema akaikusanya na kuiweka sehemu
moja ili iunganike na takataka nyingine kwaajili ya matumizi mengine ama
kufanyiwa recycling)
Faida
nyingine ya mabwawa haya huruhusu ufugaji kufanyika katika eneo dogo kwa unadhifu Zaidi.Hii hufungua fursa ya
ufugaji wa samaki kwa wakazi waishio katikati ya miji wenye maeneo madogo.
UDHAIFU WA UJENZI HUU WA MABWAWA:
Mfugaji
asipokua makini wakati wa uchaguzi wa turbai anaweza pata turbai zilizo chini
ya kiwango na kuleta usumbufu wa kupasuka na kuvujisha maji mara kwamara.
Pia
plastic ina sifa ya kupata joto sana wakati wa jua kali hivyo kwa wafugaji
waishio maeneo ya joto akiwa
amepandikiza samaki wengi kupitiliza ndani ya eneo dogo joto liliongezeka
samaki wataathirika,ni muhimu kama ni mfugaji wa maeneo ya joto awe makini
kufuatilia mabadiliko ya hali joto ya maji kwa kupima temperature mara kwa mara
ili aweze kuzuia athari hizi.
USHAURI KWA WAFUGAJI WANAOISHI VIJIJINI,PEMBEZONI MWA HIFADHI ZA BAHARI
NA HIFADHI ZA WANYAMA PORI NA MAZINGIRA KWA UJUMLA:
Kwa matokeo chanya ya ufugaji wako na
pasipo kuleta uharibifu wa mazingira ni vizuri kutumia ufugaji huu katika hali
ya ufugaji mseto (intergrated fish farming)
kwani utakupa faida kubwa kwakua ufugaji huu mseto unaleta mtegemeano
mkubwa wa kiikolojia pia hautaaribu mazingira.
Mtegemeano wa kiikolojia unaotokea:
Unapofuga kuku ama bata pamoja na samaki
kinyesi cha kuku ama bata utakitumia kutengenezea chakula cha asili kwenye
bwawa(algae,phytoplankton,zoo plankton) lakini pia wakati wakubadili maji
kwenye bwawa badala ya kumwaga maji ovyo,maji hayo kumbuka yana virutubisho
vingi,mbolea nyingi ambayo ni nzuri sana kwenye ukuaji wa mimea hivyo
unaelekezea bomba la outlet kwenye bustani yako yaweza kuwa ya
mbogamboga,matunda,nafaka kama mahindi ama miti ya a mbao ambavyo vitakupa
faida ya chakula pia na fedha,Zaidi ya hapo unapo vuna mazao yako kama mahinndi
mabaki ya majani na magunzi hautatupa utawapatia mifugo yako kama nguruwe na
wengineo hii itakusaidia kuepukana na migogoro ya kuachia mifugo ovyo kwenda
ndani ya maeneo ya hifadhi lakini pia itakusaidia katika utunzaji mazingira
kwani utajikuta hautaacha takataka ama mabaki yeyote ovyo kwenye mazingira,kila
kitu kinakuwa na matumizi yake kwa mtegemeano huo wa kiikolojia ya viumbe
uliyoitengeneza.
Ahsante kwa kufuatilia masomo yetu,kwa msaada wowote usisite kuwasiliana nasi.